24
Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija? Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao. Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana. Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao. Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao. Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu. Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi. Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao. Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini. 10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula. 11 Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu. 12 Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao. 13 Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake. 14 Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku. 15 Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha. 16 Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru. 17 Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro. 18 Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu. 19 Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi. 20 Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti. 21 Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane. 22 Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha. 23 Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao. 24 Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka. 25 Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?”