23
Kisha Ayubu akajibu na kusema, “Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu. Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo! Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja. Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu. Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza. Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu. Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona. Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone. 10 Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu. 11 Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka. 12 Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake. 13 Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda. 14 Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo. 15 Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa. 16 Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha. 17 Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.