25
Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema, “Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni. Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake? Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye? Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake. Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!”