9
1 Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu,
2 kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu.
3 Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili.
4 Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi.
5 Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.
6 Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia. Maana si kila mtu aliye Israeli ni Mwiisraeli halisi.
7 Sivyo hata kwa uzao wa Abrahamu kuwa ni watoto wake halisi. Lakini, “ni kupitia Isaka uzao wako utaitwa.”
8 Hii ni kwamba, watoto wa mwili si watoto wa Mungu. Lakini watoto wa ahadi wanatazamwa kuwa kama uzao.
9 Maana hili ndilo neno la ahadi: “Katika majira haya nitakuja, na Sara atapewa mtoto.”
10 Si hili tu, lakini baada ya Rebeka kupata mimba kwa mtu mmoja, Isaka baba yetu-
11 kwamba watoto walikuwa bado hawajazaliwa na alikuwa hajafanya jambo lolote zuri au baya, ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisimame, wala si kwa matendo, lakini ni kwa sababu ya yule aitae.
12 Ilinenwa kwake, “Mkubwa atamtumikia mdogo.”
13 Kama ilivyo kwisha andikwa: “Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.”
14 Basi tena tutasema nini? Je kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha.
15 Kwa kuwa anasema kwa Musa, “nitakuwa na rehema kwa yule nitakayemrehemu, na nitakuwa na huruma kwa yule nitakayemhurumia.”
16 Kwa hiyo basi, si kwa sababu ya yeye atakaye, wala si kwa sababu ya yeye ambaye hukimbia, lakini kwa sababu ya Mungu, ambaye huonesha rehema.
17 Kwa kuwa maandiko husema kwa Farao, “Kwa kusudi hili maalumu nilikuinua, ili kwamba nioneshe nguvu zangu katika wewe, na ili kwamba jina langu litangazwe katika nchi yote.”
18 Hivyo basi, Mungu huwa na rehema kwa yeyote ampendaye, na kwa ambaye humpenda, humfanya kuwa mkaidi.
19 Kisha utasema kwangu, “Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?”
20 Kinyume chake, mwanadamu, wewe ni nani ujibue kinyume na Mungu? Kuna uwezekano wowote wa kilichofinyangwa kusema kwa mfinyanzi, “Kwanini ulinifanya hivi mimi?”
21 Je mfinyazi huwa hana haki juu ya udongo kutengeneza chombo kwa matumizi maalumu kutokana na bonge lile lile, na chombo kingine kwa matumizi ya kila siku?
22 Vipi kama Mungu, ambaye ana utayari wa kuonesha gadhabu yake na kufanya nguvu yake kujulikana, alistahimili kwa uvumilivu wa kutosha vyombo vya gadhabu vilivyoandaliwa kwa kuangamiza?
23 Vipi kama alifanya hivi ili kwamba aoneshe wingi wa utukufu wake juu ya vyombo vya rehema, ambavyo alikwisha kuviandaa kwa ajili ya utukufu?
24 Vipi kama alifanya hii pia kwetu, ambaye pia alituita, si tu kutoka kwa Wayahudi, lakini pia kutoka kwa watu wa Mataifa?
25 Kama asemavyo pia katika Hosea: “Nitawaita watu wangu ambao hawakuwa watu wangu, na mpendwa wake ambaye hakupendwa.
26 Na itakuwa kwamba pale iliposemwa kwao, 'Ninyi si watu wangu,' pale wataitwa 'wana wa Mungu aliye hai.”'
27 Isaya analia kuhusiana na Israeli, “Kama hesabu ya wana wa Israeli ingekuwa kama mchanga wa bahari, itakuwa ni masalia ambao wataokolewa.
28 Kwa kuwa Bwana atalichukua neno lake juu ya nchi, mapema na kwa utimilifu.
29 Na kama jinsi Isaya alivyosema awali, “Kama Bwana wa majeshi hakutuachia nyuma uzao kwa ajili yetu, tungekuwa kama Sodoma, na tungefanywa kama Gomora.
30 Tutasema nini basi? kwamba watu wa Mataifa ambao walikuwa hawatafuti haki, walipata haki, haki kwa imani.
31 Lakini Israeli, ambaye alitafuta sheria ya haki, hakuifikia.
32 Kwanini si hivyo? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani, bali kwa matendo. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa,
33 kama ilivyo kwisha andikwa, “Tazama, nimelaza jiwe la kujikwaa katika Sayuni na mwamba wa kukosa. Yeye ambaye huamini katika hili hataaibika.”