17
1 Ikawa baada ya mfalme kuwa katika nyumba yake, akasema kwa Nathani yule nabii, “Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema.”
2 Kisha Nathani akasema kwa Daudi, Nenda, fanya yalio moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yupo nawe.”
3 Lakini usiku huo neno la Mungu lilimjia Nathani, nakusema,
4 “Nenda umwambie Daudi mtumishi wangu, 'Hivi ndivyo Yahweh asemavyo: Hautanijengea nyumba ya kuishi.
5 Kwa kuwa sijaishi katika nyumba toka ile siku niliyo ileta Israeli hadi leo. Badala yake, nimeishi ndani ya hema, hema la kukusanyikia, sehemu mbali mbali.
6 Katika sehemu zote nilizo enda na Israeli, niliwai kusema lolote kwa viongozi wa Israeli niliyo wachagua kuwa chunga watu wangu, kwa kusema, “Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierezi?””
7 “Kisha sasa, mwambie mtumishi wangu Daudi, 'Hili ndilo Yahweh wa majeshi anasema: Nilikuchugua kutoka malishoni, kufuata kondoo, ilikwamba uwe mtawala wa watu wangu Waisraeli.
8 Nimekuwa nawe pote ulipo enda na nimewakata maadui zako wote, na na nitakufanyia jina, kama jina la wakuu wa dunia.
9 Nitachagua sehemu ya watu wangu Israeli na nitawapanda hapo, iliwaishi sehemu yao na wasisumbuke tena. Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya mwanzo,
10 kama walivyo kuwa wakifanya toka siku zile nilipo waamuru waamuzi kuwa juu ya watu wangu Waisraeli. Kisha nitawatiisha maadui zako wote. Zaidi sana nina kwambia kwamba mimi, Yahweh, nitakujengea nyumba.
11 Itakuja kuwa hapo siku zako zitapo timia za wewe kwenda kwa baba zako, nitainua uzao wako baada yako, na mmoja wa uzao wako nitaimarisha ufalme wake.
12 Yeye atanijengea nyumba, na nitaimarisha kiti chake cha enzi milele.
13 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana wangu. Sitaondoa uwaminifu wa Agano langu kwake, kama nilivyo ondoa kwa Sauli, aliye tawala kabla yako.
14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.”
15 Nathani akanena haya kwa Daudi na kumtaarifu, na akamwambia kuhusu maono yote.
16 Kisha Daudi mfalme akaenda ndani na kuketi mbele za Yahweh; akasema, “Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?
17 Hili lilikuwa jambo dogo machoni pako, Mungu. Umezungumzia familia ya mtumishi wako kwa muda mrefu ujao, na umenionyesha vizazi vijavyo, Yahweh Mungu.
18 Nini zaidi mimi, Daudi, niseme? Umemheshimu mtumishi wako. Umemtambua kwa kipekee mtumishi wako.
19 Yahweh, kwa ajili ya mtumishi wako, na kutimiza kusudi lako, umefanya hili ilikudhihirisha matendo yako makuu.
20 Yahweh, hakuna aliye kama wewe, na hakuna Mungu zaidi yako, kama tulivyo sikia mara zote.
21 Ni taifa gani duniani kama watu wako Israeli, ambaye wewe, Mungu, uliwaokoa kutoka Misri iliwawe watu wako, kujifanyia jina lako kwa matendo makuu na yahajabu? Uliondoa mataifa mbele za watu wako, uliye waokoa kutoka Misri.
22 Ulifanya Israeli watu wako milele, na wewe, Yahweh, ukawa Mungu wao.
23 Hivyo sasa, Yahweh, ile ahadi uliyo iweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake itimizwe milele. Fanya kama ulivyo nena.
24 Jina lako na litukuzwe milele na kuwa kuu, ili watu waseme, 'Yahweh wa majeshi ni Mungu wa Israeli,' na nyumba yangu, mimi Daudi, mtumishi wako ikiwa imeimarishwa mbele zako.
25 Kwa kuwa wewe, Mungu wangu, umedhihirisha kwa mtumishi wako utamjengea nyumba. Hiyo ndio sababu, mimi mtumishi wako, nimepata ujasiri wa kuomba kwako.
26 Sasa, Yahweh, wewe ni Mungu, na umefanya hii ahadi nzuri kwa mtumishi wako:
27 Sasa imekupendeza kubariki nyumba ya mtumishi wako, iliiendelee milele mbele zako. Wewe, Yahweh, umeibariki, na itabarikiwa milele.”