75
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Asafu, wimbo.
1 Tunatoa shukrani kwako, Mungu; tunatoa shukrani, maana wewe unaufunua uwepo wako; watu huzungumza kuhusu kazi zako za ajabu.
2 Kwa wakati maalum nitahukumu kwa haki.
3 Ingawa nchi na wenyeji wote watatikisika katika hofu, ninaifanyia nchi nguzo za kutosha. Selah
4 Nilisema kwa wenye kiburi, “Msiwe wenye kiburi,” na kwa waovu, “Msiinue mapembe.
5 Msiinue mapembe yenu kwenye marefu; wala msizungumze kwa shingo ya kiburi.”
6 Sio kutoka mashariki au magharibi, na wala sio kutoka jangwani ambako kuinuliwa kunakuja.
7 Bali Mungu ni muhumkumu; humshusha huyu na kumuinua huyu.
8 Kwa kuwa Yahwe kashikilia mkononi mwake kikombe cha mvinyo wenye povu, ambao umechanganywa na vilolezo, naye huimimina. Hakika waovu wote wa duniani watakunywa mvinyo hadi tone la mwisho.
9 Bali mimi nitaendelea kusema yale ambayo umeyatenda; nami nitamwimbia sifa Mungu wa Yakobo.
10 Yeye husema, “Nitayakata mapembe yote ya waovu, lakini mapembe ya wenye haki yatainuliwa.”