57
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi; wakati alipo mkimbia Sauli, pangoni.
1 Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
2 Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu.
3 Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. Selah Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake.
4 Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga.
5 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu, utukufu wako uwe juu ya nchi yote.
6 Wao walisambaza nje wavu kwa ajili ya miguu yangu; nilikuwa na shida sana. Walichimba shimo mbele yangu. Wao wenyewe wameangukia katikati ya shimo! Selah
7 Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa.
8 Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
9 Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa.
10 Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni.
11 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.