52
Kwa kiongozi wa muziki. Maschil ya Daudi; wakati Doegi Mwedomi alipokuja na kumwambia Sauli, na kumwambia yeye, “Daudi amekuja kwenye nyumba ya Ahimeleki.”
1 Kwa nini wewe unajivunia kufanya uovu, wewe mtu mwenye nguvu? Uaminifu wa agano la Mungu huja kila siku.
2 Ulimi wako hupanga uharibifu kama wembe mkali, na kufanya udanganyifu.
3 Wewe unapenda uovu kuliko wema na udanganifu kuliko kuongea haki. Selah
4 Wewe hupenda maneno ambayo huwaumiza wengine, wewe ulimi mdanganyifu.
5 Vivyo hivyo Mungu atakuadhibu wewe milele; yeye atakuchukua na kukuondoa katika hema yako na kukung'oa katika ardhi ya uhai. Selah
6 Wenye haki pia wataona na kuogopa; watamcheka na kusema,
7 “Tazama, huyu ni mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa kimbilio lake la usalama, bali aliamini katika wingi wa mali zake, naye alikuwa na nguvu alipowaharibu wengine.”
8 Lakini kwangu mimi, niko kama mti bora wa mzeituni katika nyumba ya Mungu; Nami nitaamini uaminifu wa agano la Mungu milele na milele.
9 Nitakushukuru wewe daima kwa uliyo tenda. Nitalisubiri jina lako, kwa sababu ni zuri, uweponi mwa wantu wako wa kimungu.