46
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya mwana wa Korah; seti kwenye Alamoth. Wimbo.
1 Mungu kwetu ni kimbilio la usalama na nguvu, upatikanao tele wakati wa mateso.
2 Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu,
3 hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. Selah
4 Kuna mto, mikondo yake huufanya mji wa Mungu kufurahi, mahali patakatifu pa hema ya Aliye Juu.
5 Mungu yuko katikati yake; naye hatasogezwa; Mungu atamsaidia, naye atafanya hivyo asubuhi na mapema.
6 Mataifa yalikasirika na falme zikataharuki; yeye alipaza sauti yake, na nchi ikayeyuka.
7 Yahwe wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Selah
8 Njoni, mtazame matendo ya Yahwe, uharibifu alioufanya juu ya nchi.
9 Anaisitisha vita kwenye nchi; yeye anauvunja upinde na kuikata vipande vipande mishale; anazichoma ngao.
10 Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi.
11 Mungu wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Serah