3
Zaburi ya Daudi, wakati alipo mkimbia mtoto wake Absalom.
1 Yahewh, maadui zangu wako wangapi! Ni wengi wamekuja kinyume na mimi.
2 Ni wengi wanaonisema, “Hakuna msaada wowote kutoka kwa Mungu kwa ajili yake.” Selah
3 Bali wewe, Yahweh, u ngao yangu pande zote, utukufu wangu, na uniinuaye kichwa changu.
4 Nampazia Yahweh sauti yangu, na yeye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu.
5 Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda.
6 Sitaogopa kusanyiko la watu ambao wamejipanga kinyume na mimi pande zote.
7 Inuka, Yahweh! Uniokoe, Mungu wangu! Kwa kuwa utawapiga maadui zangu wote kwenye taya zao; utayavunja meno ya waovu.
8 Wokovu unatoka kwa Yahweh. Baraka zako ziwe juu ya watu wako.