126
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.
2 Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.”
3 Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo!
4 Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini.
5 Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.
6 Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.