123
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni.
2 Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia.
3 Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana.
4 Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.