12
Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye Sheminith. Zaburi ya Daudi.
1 Msaada, Yahweh, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; nao waaminifu wametokomea.
2 Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu.
3 Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa.
4 Hawa ni wale ambao wamesema, “Kwa ndimi zetu tutashinda. Wakati midomo yetu itakapo ongea, ni nani atakaye kuwa mtawala juu yetu?”
5 “Kwa sababu ya vurugu zilizopo kinyume na maskini, na kwa sababu ya kuugua kwao wahitaji, Nitainuka,” asema Yahwe. “Nitawaletea usalama wanao hitaji.”
6 Maneno ya Yahwe ni masafi, kama fedha iliyo safishwa katika tanuru duniani, iliyo ng'arishwa mara saba zaidi.
7 Wewe ni Yahwe! Unaye watunza. Una wahifadhi wacha Mungu kutoka katika hiki kizazi cha waovu na hata milele.
8 Waovu hutembea kila pande pale uovu unapoinuliwa kati ya wanadamu.