118
1 Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2 Israeli na aseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
3 Nyumba ya Haruni na iseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
4 Wafuasi waaminifu wa Yahwe na waseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
5 Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe; Yahwe alinijibu na kuniweka huru.
6 Yahwe yuko pamoja nami; sitaogopa; mwanadamu atanifanya nini? Yahwe yuko upande wangu kama msaidizi;
7 nitawatazama kwa ushindi wale walio nichukia.
8 Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu.
9 Ni bora kukimbilia katika Yahwe kuliko kuamini katika wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
11 Walinizunguka; naam, walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
12 Walinizunguka kama nyuki; walitoweka haraka kama moto kati ya miiba; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
13 Walinishambulia ili waniangushe, lakini Yahwe alinisaidia.
14 Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu, na ndiye anaye niokoa.
15 Kelele za ushindi zimesikika katika maskani ya wenye haki; mkono wa kuume wa Mungu umeshinda.
16 Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda.
17 Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe.
18 Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife.
19 Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe.
20 Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo.
21 Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu.
22 Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi.
23 Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu.
24 Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.
25 Tafadhali, Yahwe, utupe ushindi! Tafadhali, Yahwe, utupe mafanikio!
26 Amebarikiwa yule ajaye katika jina la Yahwe; tunakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe.
27 Yahwe ni Mungu, na ametupa sisi nuru; ifungeni dhabihu kwa kamba pembeni mwa madhabahu.
28 Wewe ni Mungu wangu, nami nitakushukuru; wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe.
29 Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema; kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.