110
Zaburi ya Daudi. 
1 Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”  
2 Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako.  
3 Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande.  
4 Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.”  
5 Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme.  
6 Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi.  
7 Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu.