10
1 Kwa nini, Yahweh, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida?
2 Kwa sababu ya majivuno yao, watu waovu waawakimbiza wanyonge; Basi tafadhari uwafanye waovu kunaswa kwa mipango yao wenyewe walioipanga.
3 Kwa kuwa mtu mwovu hujivuna kwa tamaa yake ya ndani; yeye hufurahisha tamaa na kumtusi Yahweh.
4 Mtu mwovu ameinua uso wake; naye hamtafuti Mungu. Yeye hamfikilii Mungu kamwe kwa kuwa hamjali kabisa Mungu.
5 Yeye yuko salama wakati wote, amri zako za haki ziko juu sana kwake; naye huwadharau adui zake wote.
6 Yeye husema moyoni mwake, “Siwezi kamwe kushindwa; katika kizazi chote sitakutana na shida.”
7 Mdomoni mwake kumejaa kulaani na udanganyifu, maneno yenye sumu; ulimi wake unajeruhi na kuharibu.
8 Yeye husubilia kwenye shambulio karibu na kijiji; mahali pa siri huwauwa watu wasio na hatia; macho yake huwatazama wasionahatia.
9 Hujibanza mahari pa siri kama simba katika kichaka; yeye hulala akisubiri kumkamata mnyonge. Humkamata pale anapokwisha mweka mtegoni mwake.
10 Wanyonge wake hugandamizwa chini na kupigwa; wao huangukia katika mtego imara.
11 Yeye husema katika moyo wake, “Mungu amesahau; huficha uso wake; hawezi kujishughulisha kutazama.”
12 Inuka, Yahweh! Inua mkono wako, Mungu! Usiwasahau wanyonge.
13 Kwa nini mtu mwovu anamkataa Mungu na kusema moyoni mwake, “Hautanipata katika hatia?”
14 Umeona, maana mara zote unaangalia mtu aletaye madhara na jeuri. Mtu asiye na msaada hukuachia nafsi yake; maana wewe huwaokoa yatima.
15 vunja mkono wa mwovu lo na mtu mwovu. Umuajibishe kwa matendo yake maovu, ambayo kwayo alifikiri hautayagundua.
16 Yahweh ni mfalme milele daima; mataifa yanaondolewa katika aridhi yake.
17 Yahweh, umesikia uhitaji wa wanyonge; nawe umeitia nguvu mioyo yao, wewe unasikia maombi;
18 Unawatetea yatima na wanyonge ili kusudi pasiwepo na mtu katika dunia hii atakaye leta hofu tena.