2
Ikiwa kuna kutiwa moyo katika Kristo. Ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake. Ikiwa kuna ushirika wa Roho. Ikiwa kuna rehema na huruma. Ikamilisheni furaha yangu kwa kunia mamoja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja. Msifanye kwa ubinafsi na majivuno. Isipokuwa kwa unyenyekevu mkiwaona wengine kuwa bora zaidi yenu. Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine. Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu. Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho. Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu. Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba. Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina. 10 Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi. 11 Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. 12 Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka. 13 Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye. 14 Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano. 15 Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu. 16 Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure. 17 Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote. 18 Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami. 19 Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu. 20 Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu. 21 Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo. 22 Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili. 23 Kwa hiyo ninatumaini kumtuma haraka pindi tu nitakapofahamu nini kitatokea kwangu. 24 Lakini nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja hivi karibuni. 25 Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu. 26 Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa. 27 Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni. 28 Kwa hiyo ninamrejesha kweny haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi. 29 Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye. 30 Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwa mko mbali nami.