2 Petro
1
Simon Petro, Mtumwa na Mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale walioipokea imani ile ile ya thamani kama tulivyoipokea sisi, imani iliyo ndani ya haki ya Mungu na mwokozi wetu Yesu Kristo. Neema iwe kwenu; amani iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Bwana wetu Yesu. Kupitia maarifa ya Mungu tumepata mambo yake yote kwa ajili ya uchaji wamaisha, Toka kwa Mungu aliyetuita kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake. Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warith wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii. Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri kwa njia ya imani yenu, kwa sababu ya uzuri, maarifa. Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa. Kupitia utauwa upendo wa ndugu na kupitia upendo wa ndugu, upendo. Kama mambo haya yamo ndani yenu, yakiendelea kukua ndani yenu, basi ninyi hamtakuwa tasa au watu msiozaa matunda katika maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo. Lakini yeyote asiyekuwa na mambo haya, huyaona mambo ya karibu tu; yeye ni kipofu. amesahau utakaso wa dhambi zake za kale. 10 Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu. Kama mtayafanya haya, hamtajikwaa. 11 Hivyo mtajipatia wingi wa lango la kuingilia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo. 12 Kwa hiyo mimi nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya kila mara, hata kama mnayafahamu, na sasa mmekuwa imara katika kweli. 13 Nafikiria kuwa niko sahihi kuwaamsha na kuwakumbusha juu ya mambo haya, ningali nimo katika hema hii. 14 Kwa maana najua kuwa si muda mrefu nitaiondoa hema yangu, kama Bwana Yesu Kristo alivyonionyesha. 15 Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya baada ya mimi kuondoka. 16 Kwa kuwa sisi hatukufuata hadthi zilizoingizwa kwa ustadi pale tulipowaeleza juu ya nguvu na kujidhihirisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, bali sisi tulikuwa mashahidi wa utukufu wake. 17 Yeye alipokea Utukufu na heshima toka kwa Mungu baba pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ndiye mwanangu, mpendwa wangu ambaye nimependezwa naye.” 18 Tuliisikia sauti hii ikitokea mbinguni pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu. 19 Tunalo hili neno la unabii lililothibitika, ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza. Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kuchapo na nyota za mawio zionekanazo katika mioyo yenu. 20 Tambueni haya ya kwamba, hakuna unabii unaoandikwa kwa sababu ya kujifikirisha kwa nabii mwenyewe. 21 Kwa kuwa hakuna unabii uliokuja kwa mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu.