22
Watu wa Israeli wakasafiri mpaka wakaweka kambi kwenye uwanda wa Moabu karibu na Yeriko, kwenye upande mwingine wa mto Yorodani kutoka mji ule. Balaki mwana wa Zippori aliona yote ambayo Israeli aliwafanyia Waamori. Moabu aliogopa sana hao watu kwa sababu walikuwa wengi sana, na Moabu alIwahofia wana wa Israeli. Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, “Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho na maksai hula nyasi za kondeni.” Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu. Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, “Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi. Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa.” Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki. Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo. Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?” 10 Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema, 11 'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'” 12 Mungu akamjiu Balaam, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.” 13 Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki,. “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.” 14 Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.” 15 Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali. 16 Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, “Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, 'Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu, 17 kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.'” 18 Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, “Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia. 19 Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia.” 20 BWANA akaja kwa Balaamu usiku ule na kumwambia, “kwa kuwa hawa watu wamekuja kukuita, inuka uende nao. Lakini utafanya tu kile nitakachokuambia kufanya.” 21 Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu. 22 Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye. 23 Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani. 24 Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta. 25 Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda. 26 Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine. 27 Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake. 28 Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?” 29 Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.” 30 Yule punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?” Balaamu akasema “hapana.” 31 Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini. 32 Yule malaika wa BWANA akamwambia, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu. 33 Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai. 34 Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, nimetenda dhambi. Sikujua kuwa ulisimama kinyume na mimi barabarani. Kwa hiyo sasa, kama haikupendezi, Nitageuka.” 35 Lakini yule malaika wa BWANA akamwambia Balaamu, “endelea na wale watu. Lakini utasema maneno nitakayokwambia tu.”Kwa hiyo Balaamu akaendelea na wale vioingozi wa Balaki. 36 Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, ambao uko mpakani. 37 Balaki akamwambia Balaamu, “Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?” 38 Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu.” 39 Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi. 40 Kisha Balaki akatoa sadaka ya maksai na kondoo na kumpatia Balaamu baadhi ya hiyo nyama na wale viongozi waliokuwa pamoja naye. 41 Kesho yake asubuhi, Balaki akampeleka Balaamu mpaka juu mahali pa Baali. Kule juu Balaamu aliweza kuona sehemu tu ya kambi za Waisraeli.