18
1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
2 “Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
3 Msitende mambo ambayo watu wa Misri huyatenda, mahali mlikokuwa mkiishi awali. Na ni lazima msitende mambo yale wanayoyatenda watu wa Kanaani, nchi ambayo ninawapeleka nyinyi. Msifuate desturi zao.
4 Sheria zangu ndizo mtakazozitenda, na amri zangu ndizo mtakazozishika, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
5 Kwa hiyo ni lazima mzitunze hukumu zangu na sheria zangu. Ikiwa mtu amezitii, ataishi kwa sababu ya hizo. Mimi Ndimi Yahweh.
6 Pasiwepo kwenu atakayelala na yeyote aliye na uhusiano wa karibu naye. Mimi ndimi Yahweh.
7 Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye.
8 Usilale na yeyote wa wake za baba yako; Usimfedheheshe namna hiyo baba yako.
9 Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.
10 Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.
11 Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.
12 Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.
13 Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.
14 Usimfedheheshe ndug wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.
15 Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
16 Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
17 Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
18 Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
19 Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
20 Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
21 Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
22 Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
23 Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
24 Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
25 Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
26 Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
27 Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
28 Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
29 Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.
30 Kw a hiyo inawapasa kuzishika amri zangu na sitende mojawapo ya desturi hizi zenyekuchukiza ambazo zilitendwa hapo kabla yenu, ili msijinajisi wenyewe kwa hizo. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.