10
1 Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua kila mtu kifukizo chake, akaweka moto ndani yake, na kisha uvumba. Kisha wakatoa moto usiokuabalika mbele za Yahweh, moto ambao hakuwaamru wao kuutoa.
2 Kwa hiyo moto ukashuka chini mbele za Yahweh na kuwala, nao wakafa mbele za Yahweh.
3 Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'” Naye Aroni hakusema neno lolote.
4 Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Aroni, naye akamwambia, “njoo huku na uwatowe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema.”
5 Hivyo wakakaribia na kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani, nao wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyokuwa ameelekeza. Kisha Musa akamwambia Aroni na wanawe wengine wawili, Eliezari na Ithamari, “
6 Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahweh asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto.
7 Msiende nje kutoka kwenye ingilio la hema la kukutania, ama sivyo mtakufa, kwa kuwa mafuta ya Yahweh ya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakatenda sawasawa na maelekezo ya Musa.
8 Mungu akazungumza na Aroni, akisema,
9 “Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,
10 ili kupaambanua kati ya mambo matakatifu na mambo ya kawaida, na kati ya najisi na safi,
11 ili kwamba mweze kuwafundisha watu wa Israeli amri zote ambazo Yahweh ameziamru kwa kinywa cha Musa.
12 Musa akazungumza na Aroni na wanawe wawili waliosalia; Eliazari naIthamari, Twaeni sadaka ya nafaka inayobaki kutokana na sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto, nanyi ileni kando ya madhabahu bila hamiara, kwa kuwa ni takatifu sana.
13 lazima mtaila mahali patatifu kwa sababu huo ni mgao wako wewe na mgao wa wanao wa matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, kwa kuwa hivi ndivyo limeamriwa niwaambie.
14 Kile kidari kitikiswacho na lile paja ambalo hutolewa kwa Yahweh, yapasa mzile mahali palipo safi panapokubalika kwa Mungu. Wewe mwenyewe, wanao na binti zako waliopamoja nawe mtakula sehemu hizo, kwa kuwa zimetolewa kuwa mgao wako na mgao wa wanao kutokana na dhabihu ya sadaka ya ushirika wa watu wa Israeli.
15 Lile paja lililotolewa na kidari kilichotikiswa, ni lazima ziletwe pamoja na sadaka ya mafuta iliyofanywa kwa moto, ili kutikiswa mbele za Yahweh. Nazo zitakuwa zako wewe na wanao kuwa mgao wenu daima, kama Yahweh alivyoamru.
16 Kisha Musa akauliza kuhusu yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye akagundua kwamba alikuwa ametekezwa kwa moto. Kwa hiyo akawakasirikia Eliazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia; akawaambia,
17 “Kwa nini hamjaila sadaka ya dhambi katika eneo la hema, kwa kuwa ni takatifu sana, na kwa kuwa Yahweh amishaitoa kwenu ili kuchukua uovu wa kusanyiko, ili kufanya upatanisho kwa aijli yao mbele zake?
18 Tazama, damu yake haikuletwa ndani ya hema, kwa hiyo iliwapasa kwa hakika kuwa mekwisha ila kwenye eneo la hema, kama nilivyoagiza?
19 Kisha Aroni akamjibu Musa, “ Tazama, leo walitoa sadaka yao ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa mbele za Yahweh, na jambo hili vilevile limetendeka kwangu leo. Ikiwa nimeshakula sadaka ya dhambi leo, Je! Isingekuwa imeshapendeza mbele za Yahweh?”
20 Naye Musa aliposikia hivyo, akaridhika.