21
1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hefziba.
2 Alifanya maovu usoni kwa Yahwe, kama machukizo ya mataifa ambayo Yahwe aliyafukuza nje mbele ya wana wa Israeli.
3 Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.
4 Manase akajenga madhabahu za kipagani kwenye nyumba ya Yahwe, ingawaje Yahwe aliamuru, “Jina langu litakuwa Yerusalemu daima.”
5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Yahwe.
6 Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao ushirikina na kujishuhulisha pamoja wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni kwa Yahwe na kuchochea hasira kwa Mungu.
7 Sanamu ya kuchongwa ya Ashera ambayo aliitnegeneza, akaiweka kwenye nyumba ya Yahwe. Nyumba hii ndiyo ambayo Yahwe alimwambia Daudi na Sulemani mwanawe; alisema: “Ni nyumba hii na katika Yerusalemu, ambayo nimeichagua kutoka makabila yote ya Isaraeli, ambako nitaliweka jina langu milele.
8 Sintofanya miguu ya Israeli kushindwa tena nje ya nchi ambayo niliwapa babu zao, kama tu watakuwa makini kutii yale yote niliyowaamuru, na kufuata sheria zote ambazo mtumishi wangu Musa aliwaamuru.”
9 Lakini watu hawakusikia, na Manase akawaongoza kufanya maovu zaidi kuliko yale ya mataifa ambayo Yahwe aliyaharibu mbele ya watu wa Israeli.
10 Basi Yahwe akaongea na watumishi wake manabii, akisema,
11 Kwasababu Manase mfalme wa Yuda amefanya haya machukizo, na kutenda maovu zaidi kuliko yote waliyoyatenda Waamori ambao walikuwa mbele yake walikubali, na pia aliwafanya Yuda kuasi kwa sanamu zake,
12 kwa hiyo Yahwe, Mungu wa Israeli, akasema hivi: Tazama, nakaribia kuleta uovu juu ya Yerusalemu na Yuda ambayo kila mtu asikiapo kuhusu hilo, masikio yake yote yatang'aa.
13 Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kipimo kilichotumika dhidi ya Samaria, na kuangusha msatari utakaotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu; Nitaifuta Yerusalemu safi, kama kufuta sahani, kuifuta na kuifunika juu chini.
14 Nitawatupa masalia ya urithi wangu na kuwaweka mikononi mwa maadui zao. Watakuwa nyara na mateka kwa maadui zao wote,
15 kwa sababu wamefanya yaliyo maovu usoni kwangu, na kunichochea hasira, tangu siku babu zao walipotoka Misri, hadi leo.”
16 Aidha, Manase akazimwaga damu nyingi za wasio na hatia, hadi alipoijaza Yerusalemu kutoka upande huu kwenda mwingine kwa kifo. Hii ilikuwa ni kuongeza kwenye dhambi ambayo aliifanya Yuda kuasi, wakati walipofanya uovu mbele za Yahwe.
17 Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Manase, yote aliyoyafanya, na dhambi ambayo aliyoifanya, je haya hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?
18 Manase akalala pamoja na babu zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
19 Amoni alikuwa na miaka kumi na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Meshlemethi; alikuwa binti wa Haruzi wa Yotba.
20 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama manase baba yake alivyofanya.
21 Amoni alifuata njia zote ambazo baba yake alizotembelea na kuabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu, na kuzisujudia.
22 Akajitenga na Yahwe, Mungu wa baba zake, na hakutembea katika njia ya Yahwe.
23 Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
24 Lakini watu wa nchi wakawaua watu wote waliofanya njama dhidi ya mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia mtoto wake kuwa mfalme katika sehemu yake.
25 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Amoni yale aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
26 Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.