7
1 Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake.
2 Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upanawake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo.
3 Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano.
4 Nayo mihimili ilikuwa safu tatu, na kila dirisha lilikabili dirisha lingine katika madaraja matatu.
5 Milango yote na miimo ilitengenezwa kwa mraba, na madirisha yalikuwa yakikabiliana katika madaraja matatu
6 Akatengeneza baraza lenye uerfu wa mita 23 na upana wa mita 14. Mbele yake kulikuwa na ukumbi ulioezekwa.
7 Sulemani akajenga baraza yenye kiti cha enzi ambacho alitolea hukumu ya haki. Nayo ilikuwa imeezekwa kwa mwerezi kutoka sakafu moja hadi nyingine.
8 Nyumba ya Sulemani ambayo alikusudia kuishi, katika behewa nyingine ndani ya sehemu ya chini ya ikulu, ilitengenezwa kwa kazi hiyo hiyo. Pia alimjengea binti wa Farao nyumba kama hii, ambaye alikuwa mke wake
9 Majengo haya yalipmbwa kwa vitu vya thamaini, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza.
10 Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3. 7 na mengine mita 4. 8.
11 Kwa juu ilipambwa kwa, mawe ya thamani yaliyochongwa sawa sawa kwa msimeno na kwa mihimili ya mierezi.
12 Na behewa kubwa iliyokuwa ikizunguka ikulu ilikuwa na safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi kama ilivyo kwenye baraza la ndani la hekalu la BWANA na ule ukumbi wa hekalu.
13 Mfalme Sulemani alituma watu kumleta Huramu kutoka Tiro.
14 Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.
15 Huramu alizilemba zile nguzo mbili za shaba, kila moja ilikuwa na kimo cha mita 8. 3 na mzingo wa mita 5. 5.
16 Akatengeneza taji mbili za shaba za kuwekwa juu ya zile nguzo. Kimo cha kila taji ilikuwa mita 2. 3.
17 Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa ajili ya kuvipamba vile vichwa vya nguzo, nayo yailikuwa saba kwa kila kichwa.
18 Kwa hiyo Huramu akafanya safu mbili za komamanga kuzunguka vile vichwa vya nguzo ili kuvipamba vile vichwa.
19 Zile taji kwenye vile vichwa vya nguzo za ukumbi zilikuwa zimepambwa kwa maua, yenye vimo vya mita 1. 8.
20 Hizo taji kwenye hizo nguzo mbili kwenye vichwa vyake, karibu yake kulikuwa na makomamanga mia mbili yote yakiwa kwenye safu.
21 Alisimamisha nguzo kwenye ukumbi wa hekalu. Ile nguzo ya kuume akaipa jina la Yakini, na ile ya kushoto akaipa jina la Boazi.
22 Na juu ya zile nguzo kulikuwa na mapambo kama maua. Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa.
23 Tena akafanya bahari ya kusubu ya, yenye mita 2. 3 kutoka ukingo hadi ukingo, kimo chake kilikuwa mita 4. 6, mziingo wake ulikuwa mita 13. 7.
24 Na chini ya ile bahari kulikuwa na vibuyu vilivyoizunguka, vilikuwa vibuyu kumi na nane katika kila mita, vilivyowekwa katika kila hicho kipande wakati bahari inapokuwa kalibu.
25 Bahari ikakaa juu ya makisai kumi na mbili, tatu, zilitazama kaskazini, tatu zikitazama magharibi, tatu zikitazama kusini na tatu zikitazama kaskazini. Ile bahari iliwekwa juu yao, na pande zao zote za nyuma zilikuwa ndani.
26 Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwakama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi huingia bathi elfu mbili za maji.
27 Huramu akatengeneza makalio kumi ya shaba. Kila kalio lilkuwa na urefu wa mita 1. 8, upana wa mita 1. 8, na kimo cha mita 1. 3.
28 Hivi ndivyo kazi za makalio zilivyofanywa. Yalikuwa na papi ambazo zilikaa kati kati ya vipandio,
29 na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi. Chini na juu simba kulikuwa na masongo ya kazi ya kufuliwa.
30 Kila kalio lilikuwa na magurudumu ya shaba na vipini, na pande zake nne na miguu yake minne ilikuwa na mataruma chini ya birika. Chini ya birika yalikuweko mataruma ya kusubu yenye masongo katika kila upande.
31 Na kinywa chake kilikuwa cha kuviringana, chenye upana wa sentimita araobaini na sita, na ile taji ilikuwa na sentimita ishirini na tatu. Na kinywa chake kilikuwa na nakshi, na papi zake zilikuwa za mraba, na wala siyo za mvringo.
32 Yale magurudumu mawili yalikuwa chini ya papi, na mikono ya magurudumu yalikuwa ndani ya makalio. Kimo cha yale magurudumu kilikuwa sentimeta sitini na tisa.
33 Yale magurudumu yalikuwa kama ya gari. Mikono yake, na maduara, matindi yake, na vipande vya ndani vyote vilikuwa vya kusubu.
34 Kulikuwa na mataruma manne katika pande zake nne za makalio, yaliyokuwa yameshikamanishwa na kalio lenyewe.
35 Juu ya makalio kulikuwa na duara yenye kina cha sentimita ishirini na tatu, na juu ya makalio mashikio yake na papi zake zikiwa zimeshikamanishwa.
36 Juu ya mabamba na papi zake Huramu akachora makerubi, simba, na mitende ambayo ilifunika nafasi ya juu, nayo ilikuwa imezungukwa na masongo.
37 Alitengeneza makalio kumi kwa jinsi hii. Yote yalikuwa yametengenezwa kwa kufanana, na yalikuwa ya vipimo sawa, na sura inayofanana.
38 Huramu akatengeneza birika kumi za shaba. Birika moja liliweza kubeba bathi arobaini za maji. Kila birika lilikuwa mita 1. 8 toka birika moja hadi jingine na kulikuwa na birika moja katika kila kalio kati ya yale kumi.
39 Alitengeneza makalio tano upande wa kusini unaoelekea upande wa hekalu. Akatengeneza bahari katika upande wa mashariki, ukielekea upande wa kusini wa hekalu.
40 Huramu akatengeneza birika na koleo na besini la kunyunyizia. Kisha akamaliza kazi yote aliyofanya kwa mfalme Sulemani katika hekalu la BWANA:
41 Zile nguzo mbili, na lile besini lakawa kama taji ambalo lilikuwa juu ya zile nguzo, na nyavu mbili za mapambo za kufunika zile besini mbili za kuwa kama taji zilizokuwa juu ya nguzo.
42 Kisha akatengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu mbili za mapambo: safu mbili za makomamamanga kwa kila kazi ya nyavu kwa ajili ya kufunikia zile besini mbili kama taji iliyo juu ya nguzo,
43 yale makalio kumi, na birika kumi kwenye makalio.
44 Akatengeneza bahari na makisai kumi chini yake;
45 na masufuria, koleo, birika na vyombo vingine vyote. Huramu akivitengeneza kwa shaba iliyosuguliwa, kwa ajili ya mfalme Sulemani, na kawa ajili ya hekalu la BWANA.
46 Mfalme alivisubu katika uwanda wa Yorodani, katika udongo mfinyanzi kati ya Sukoti na Zarethani.
47 Sulemani hakuvipima vyombo vyote kwa sababu vilikuwa vingi mno kuvipima, na kwa sababu uzito wa shaba ulikuwa hauwezi kupimwa.
48 Sulemani akatengeneza mapambo yote yaliyokuwa kwenye hekalu la BWANA kwa kutumia dhahabu: Ile madhabahu ya dhahabu na ile meza ambayo iliwekwa mikate ya wonyesho.
49 Vile vinara vya dhahabu, ambavyo vitano vilikuwa upande wa kulia na vitano mkono wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vilikuwa vya dhahabu safi, na maua, na taa na koleo zilikuwa za dhahabu.
50 Vile vikombe, na makasi, mabakuri, na vijiko, na vyetezo vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi. na bawaba za dhahabu za milango ya ndani, ambazoo ndio mahali patakatifu sana, na milango ya ukumbi mkubwa, vyote vilitengenezwa kwa dhahabu.
51 Kwa njia hii, kazi yote ambayo mfalme Sulemani alifanya kwa ajili ya hekalu ilimalizika. Kwa Sulemani akaviingiza ndani yake vitu vile vilivyokuwa vimewekwa wakfu na Daudi, baba yake, na fedha na dhahabu, na mapambo, na vile vya ndani ya hazina ya BWANA.