2
1 Neno la BWANA lilinijia likisema,
2 “Nenda ukanene katika masikio ya Yerusalemu. Useme; BWANA asema hivi: Ninakumbuka agano la uaminifu la ujana wako, upendo wako wakati tulipokuwa tumechumbiana, ulipokuwa ukinihitaji kule jangwani, katika ile nchi iliyokuwa haijapandwa.
3 Israeli alikuwa ametengwa kwa BWANA, malimbuko yake ya mavuno yake! Wote waliokula malimbuko yake walikuwa na hatia! majanga yaliwajia—asema BWANA.'”
4 Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli.
5 BWANA anasema hivi, “Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu?
6 Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?
7 Lakini nilwaleta katika nchi ya Kameli, ili mle matunda yake na vitu vingine vyema! Lakini mlipokuja, mliitia unajisi nchi yangu, mliufany urithi wangu kuwa chukizo!
8 Hata makuhani hawakusema, 'BWANA yuko wapi?' na watalamu wa sheria hawakunijali mimi! wachungaji wametenda dhambi dhidi yangu. Manabii wamemtolea Baali unabii na kuvitafuta vitu ambvyo havina faida.
9 Kwa hiyo nitaendelea kuwashitaki - hili ni neno la BWANA - na nitawashitiki watoto wa watoto wenu.
10 Kwa kuvuka kwenda hadi pwani ya Kitimu na kutazama. Tuma wajumbe kwenda Kedari na tafuta uone kama kama iliwahi kutokea hapo awali vitu kama hivi.
11 Je, taifa limebadilisha miungu, hata kama haikuwa miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia.
12 Sitajabuni, enyi mbingu kwa sababu ya hili! Tetemekeni na kuogopa -asema BWANA.
13 Kwa kuwa watu wangu wametenda maovu mawili dhidi yangu: Wameziacha chemichemi za maji ya uhai kwa kuchimba mabarika kwa ajili yao, mabarika yanayovuja yasiyoweza kutunza maji!
14 Je, Israeli ni mtumwa? Kwani hakuzaliwa nyumbani? Kwa nini sasa amekuwa nyara?
15 Wanasimba wameunguruma dhidi yake. Wamepiga kelele sana na kuifanya kuwa ukiwa. Miji yake imeharibiwa na kubaki bila watu.
16 Pia watu wa Nufu na Tahapanesi watakinyoa kichwa chako.
17 Je, hamkufanya haya kwa ajili yenu mlipomwacha BWANA, wakati Mungu wenu, alipokuwa akiwaongoza njiani?
18 Kwa hiyo, kwa nini kutafuta msaada Misri na kunywa maji ya Shihori? Kwa nini kutafuta msaada Ashuru na kunywa maji ya Mto Frati?
19 Uovu wako unakukemea, na maasi yako yatakuadhibu. Kwa hiyo yafikiri hayo; tambua kuwa ni uovu na uchungu kwenu ninyi kuniacha mimi, BWANA Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu - asema BWANA wa majeshi.
20 Kwa kuwa niliivunja nira yenu mliyokuwa nayo wakati wa kale; Nilivichana vifungo vyako kutoka kwako. Lakini bado ulisema, 'Sitamtumikia!' tangu ulipopiga magoti katika kila kilima kuusogelea kila mti wenye majani mabichhi, enyi makahaba.
21 Lakini mimi mwenyewe niliwapanda kama mzabibu niliouchagua, mbegu iliyokamilika. Lakini tazama jinsi ulivyobadilika mbele yangu, na kuwa mzabibu usiofaa na mzabibu pori!
22 Kwa kuwa hata kama utajisafisha mwenyewe mtoni na kuoga kwa sabuni kali, bado dhambi yako ni madoa mbele yangu - asema BWANA Mungu.
23 Wawezaje kusema, 'Mimi sijanajisika! Mimi sjaenda kwa Mabaal?' Tazama tabia zako zilivyokuwa bondeni! Tambua kile ulichofanya, wewe ngamia mwepesi! akimbiaye katika njia yake!
24 Wewe ni punda wa mwitu, aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo usiofaa katika tamaa ya kuishi! Ni nani awezaye kumgeuza anapotafuta dume la kumpanda? Na punda dume amtafutaye hajichoshi mwenyewe. Huenda kwake wakati wa mwezi wa kupandwa.
25 Lazima uizuie miguu yako isikose kiatu na koo lako kuwa na kiu! Lakini umesema, 'Hakuna matumaini! Hapana! Nawapenda wageni nami huwatafuta!'
26 Kama aibu ya mwizi ilivyo anapokuwa amekamatwa, ndivyo aibu ya Israeli itakavyokuwa - wao, wafalme wao, malikia wao, makuhani na manabii wao!
27 Hawa ndio wale waiambiayo miti, 'Ninyi ndio baba zangu,' na mawe, 'Ninyi ndio mlinizaa.' Kwa kuwa migongo yao hunitazama na siyo nyuso zao. Hata hivyo, wakati wa shida husema, 'Amka utuokoe!'
28 Lakini iko wapi ile miungu mliyojitengenezea? Acha hao wainuke kama wanaweza kuwaokoa wakati wa shida, kwa kuwa hizo sanamu zenu zina idadi sawa na miji yenu, katika Yuda.
29 Kwa hiyo kwa nini kunituhumu kwa kufanya makosa? Ninyi nyote mmeniasi - asema BWANA wa majeshi.
30 Nimewadhibu watu wenu bure. Wala hawakutaka kurudiwa. Upanga wako umewaangamiza manabii wenu kama kama simba aangamizaye!
31 Enyi watu wa kizazi hiki! Sikilizeni neno langu, neno la BWANA! Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza nene? Kwa nini watu wangu husema, 'Acha tuzungukezunguke, hatutakuja kwako tena'?
32 Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wngu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
33 Jinsi mlivyotengeneza njia zenu vizuri ili kutafuta mapenzi. Hata mmewafundisha njia zenu wanawake waovu.
34 Damu ambayo ilikuwa ndio uhai wa watu wasio na hatia, imeonekana katika mavazi yenu. Hawa watu hawajawahi kuonekana katika matendo maovu.
35 Pamoja na mambo haya yote, wewe unaeendelea kusema kuwa hauna hatia. Kwa hakika hasira ya BWANA itageuka kutoka kwangu. 'Lakini tazama! Utahukumiwa kwa sababu, 'Sikutenda dhambi.'
36 Kwa nini mnatangatanga kwa urahisi katika njia zenu? Pia Misri itawahuzunisha sana, kama ilivyokuwa kwa Ashuru.
37 Mtaondoka hapo mkiwa mmehuzunika sana, mkiwa mmeweka mikono vichwani mwenu, kwa kuwa BWANA amemkutaa yule mliyemtumainia, kwa hiyo hamtapata msaada toka kwao,”