14
1 Neno la Bwana lilimjia Yeremia kuhusu ukame,
2 “Wayahudi waomboleze; basi milango yake ianguke. Wao wanaomboleza kwa ajili ya ardhi; Kilio chao kwa Yerusalemu kimepaa juu.
3 Wenye nguvu huwatuma watumishi wao kwa ajili ya maji. Wanapoingia kwenye visima, hawawezi kupata maji. Wote wanarudi hawajafanikiwa; Wao hufunika vichwa vyao na aibu.
4 Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
5 Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
6 Punda mwitu husimama kwenye mabonde yaliyo wazi na hupiga upepo kama mbweha. Macho yao yanashindwa kufanya kazi, kwa maana hakuna mimea.
7 Hata ingawa maovu yetu yanatushuhudia, Bwana, tenda kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu matendo yetu yasiyo na imani yamezidi; tumekutenda dhambi.
8 Matumaini ya Israeli, yule anayemwokoa wakati wa dhiki, kwa nini utakuwa kama mgeni katika nchi, kama mtu akaaye nchi ya kigeni ambaye hujinyoosha na kutumia hutumia usiku mmoja tu?
9 Kwa nini utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kama shujaa ambaye hawezi kuokoa mtu yeyote? Kwa maana wewe u katikati yetu, Bwana! Jina lako limetangazwa juu yetu. Usiondoke
10 Bwana awaambia hivi watu hawa “Kwa kuwa wanapenda kutanga tanga, hawakuzuia miguu yao kufanya hivyo.” Bwana hafurahi nao. Sasa anawakumbusha uovu wao na ameadhibu dhambi zao.
11 Bwana akaniambia, Usiombe kwa ajili ya watu hawa.
12 Maana ikiwa wanafunga, sitasikiliza kulia kwao; na wanapotoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga, sitawafurahia. Kwa maana nitawaangamiza kwa upanga, njaa, na tauni.
13 Ndipo nikasema, “Ee Bwana, Bwana! Angalia! mabii wanawaambia watu, 'Huwezi kuona upanga; hakutakuwa na njaa kwako, kwa kuwa nitakupa usalama wa kweli mahali hapa.'”
14 Bwana akaniambia, 'manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwafukuza, wala sikuwapa amri au kusema nao. Lakini maono ya udanganyifu na ya maana, uchawi wa udanganyifu unaotokana na akili zao ndicho wanachowahubiria.”
15 Kwa hiyo Bwana asema hivi, “Kwa habari ya manabii wakihubiri kwa jina langu, ambao mimi siwakutuma; wale wanaosema kuwa hakutakuwa na upanga wala njaa katika nchi hii mabii hawa wataangamia kwa upanga na njaa.
16 Na watu waliopewa utabiri watafukuzwa nje ya barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga; kwa kuwa hakuna mtu wa kuwazikas-wao, na wake zao, na wana wao, wala binti zao; kwa maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
17 Sema neno hili kwao 'Acha macho yangu yatokwe machozi, usiku na mchana. wala yasikome, kwa kuwa kutakuwa na kuanguka kwa bikira, binti ya watu wangu - jeraha kubwa lisilotibika.
18 Ikiwa nitatoka kwenye shamba basi angalia! kuna wale waliouawa kwa upanga. Na kama nitakuja mjini, basi, tazama! kuna wale walio na ugonjwa wa njaa. Hata nabii na kuhani wote wanatembea juu ya nchi bila maarifa.'”
19 Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu.
20 Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.
21 Usitukatae! Kwa ajili ya jina lako, usikifedheheshe kiti chako cha enzi cha utukufu. Kumbuka na usivunje agano lako na sisi.
22 Je, kuna miongoni mwa sanamu za mataifa yeyote zinazoweza kuifanya mbingu kutoa mvua? Je, si wewe, Bwana Mungu wetu, ambaye hufanya jambo hili? Tunatumaini kwako, kwa kuwa umefanya mambo haya yote.