21
1 Sasa watu wa Israeli walikuwa wameahidi huko Mispa, “Hakuna hata mmoja wetu atakayempa binti yake kuolewa na Mbenyamini.”
2 Ndipo watu wakaenda Betheli, wakakaa huko mbele ya Mungu hata jioni; wakalia kwa sauti kubwa.
3 Walipiga kelele, “Kwa nini, Bwana, Mungu wa Israeli, amefanya jambo hili kwa Waisraeli, kwamba moja ya makabila yetu linapotea leo?”
4 Siku iliyofuata watu waliamka mapema na wakajenga madhabahu huko na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.
5 Watu wa Israeli wakasema, “Ni nani kati ya kabila zote za Israeli hawakuja katika mkutano wa Bwana?” Kwa kuwa walikuwa wamefanya ahadi muhimu juu ya mtu yeyote ambaye hakuja kwa Bwana huko Mispa. Wakasema, “Hakika yeye atauawa.”
6 Watu wa Israeli walikuwa na huruma kwa ndugu yao Benyamini. Wakasema, “Leo hii kabila moja limekatiliwa mbali kutoka Israeli.
7 Ni nani atakayewapa wale walioachwa wake, kwa kuwa tumeahidi kwa Bwana kwamba hatuwezi kuwaruhusu yeyote kati yao aoe binti zetu?”
8 Wakasema, “Ni nani kati ya kabila za Israeli hawakuja kwa Bwana huko Mispa? Ilionekana kuwa hakuna mtu aliyekuja kwenye mkusanyiko kutoka Jabeshi-Gileadi.
9 Kwa maana watu walipokuwa wamepangwa kwa utaratibu, tazama, hakuna hata mmoja wa wenyeji wa Yabeshi Gileadi.
10 Mkutano huo uliwatuma watu kumi na wawili wa watu wao wenye ujasiri kwa maagizo ya kwenda Jabeshi-gileadi na kuwaangamiza, na kuwaua, hata wanawake na watoto.
11 “Fanya hivi unapaswa kuua kila mume na kila mwanamke aliyelala na mwanaume.”
12 Watu wale walikuta watu kati ya hao waliokaa Yabeshi-gileadi, wanawake mia nne ambao hawakulala na mwanaume, wakawapeleka kwenye kambi huko Shilo, huko Kanaani.
13 Mkutano wote ukatuma ujumbe na kuwaambia watu wa Benyamini waliokuwa kwenye mwamba wa Rimoni kwamba walikuwa wanawapa amani.
14 Wabenyamini walirudi wakati huo na walipewa wanawake wa Yabeshi Gileadi, lakini hapakuwa na wanawake wa kutosha kwa wote.
15 Watu waliomboleza kwa kile kilichotokea Benyamini, kwa kuwa Bwana alifanya mgawanyiko kati ya makabila ya Israeli.
16 Kisha wakuu wa mkutano wakasema, “Tutafanyaje ili Wabenyamini wapate wake, kwa kuwa wanawake wa Benyamini wameuawa?”
17 Wakasema, 'Lazima kuwe na urithi kwa Wabenyamini waliosalia, ili kabila lisiharibiwe kutoka Israeli.
18 Hatuwezi kuwapa wake kutoka kwa binti zetu, kwa kuwa wana wa Israeli walikuwa wametoa ahadi, 'Na alaaniwe mtu atakayempa Benyamini mke.'”
19 Wakasema, “Mnajua kuwa kuna sikukuu kwa Bwana kila mwaka huko Shilo ( ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona).
20 Wakawaagiza wana wa Benyamini, wakisema, “Nendeni, mjifiche kwa siri, na kusubiri katika mashamba ya mizabibu.
21 Tazama wakati ambapo wasichana kutoka Shilo watatoka kucheza, Tokeni nje ya mizabibu na kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo, kisha kurudi kwenye nchi ya Benyamini.
22 Wakati baba zao au ndugu zao watakapokuja kutupinga, tutawaambia, 'Tupeni neema! Waache wabaki kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita. Na ninyi hamna hatia juu ya ahadi, kwa sababu hamkuwapa wao binti zenu.'”
23 Watu wa Benyamini walifanya hivyo. Walichukua idadi ya wake waliowahitaji kutoka kwa wasichana waliokuwa wakicheza, nao wakawachukua ili wawe wake zao. Wakaenda na kurudi mahali pa urithi wao; wakajenga tena miji, na wakaishi ndani yao.
24 Kisha watu wa Israeli wakatoka mahali hapo na kwenda nyumbani, kila mmoja kwa kabila lake na ukoo, na kila mmoja kwa urithi wake mwenyewe.
25 Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli. Kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake mwenyewe.