5
1 Ita sasa; je kuna yeyote ambaye atakujibu? Utamrudia yupi katika watakatifu hao?
2 Kwa kuwa hasira huua mtu mpumbavu; wivu huua mjinga.
3 Nimemuona mtu mpumbavu akishika mzizi, lakini ghafla niliyalaani makazi yake.
4 Watoto wake wako mbali na uzima; wameangamia langoni mwa mji. Hakuna yeyote atakaye waponya.
5 Mwenye njaa hula mavuno yao; hata huyachukua katikati ya miiba. Wenye kiu huzihemea mali zao.
6 Kwa kuwa magumu hayatoki udongoni; wala taabu haichipuki katika nchi.
7 Badala yake, wanadamu huzaliwa kwaajili ya taabu, kama tu cheche za moto zirukavyo juu.
8 Lakini kwa mimi, ningemrudia Mungu mwenyewe; kwake ningeaminisha kusudi langu -
9 yeye afanyae makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu.
10 Hutoa mvua juu ya nchi, na huyapeleka maji mashambani.
11 Hufanya haya kwaajili ya kuwainua juu hao walio chini; huwapandisha sehemu salama hao waombolezao.
12 Yeye huharibu mipango ya watu wenye hila, ili mikono yao isipate mafanikio.
13 Yeye huwanasa watu wenye hekima katika matendo ya hila zao wenyewe; mipango ya watu waliogeuzwa huharibika haraka.
14 Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, na hupapasa mchana kama vile ni usiku.
15 Lakini yeye huokoa maskini kwa upanga wa vinywa vyao na mhitaji kwa mkono wa mtu mwenye nguvu.
16 Hivyo mtu maskini ana matumaini, na udhalimu hufumba kinywa chake mwenyewe.
17 Tazama, amebarikiwa mtu ambaye hutiwa adabu na Mungu; kwa sababu hiyo, usidharau uongozi wa Mwenyezi.
18 Kwa kuwa yeye hujeruhi na kisha huuguza; yeye hutia jeraha na kisha mikono yake huponya.
19 Yeye atakuokoa na mateso sita; kweli, katika mateso saba, hakuna uovu utakao kugusa.
20 Wakati wa njaa atakukomboa na kifo, na kwa uwezo wa upanga wakati wa vita.
21 Wewe utafichwa na mateso ya ulimi; na usitishike na uharibifu utakapokuja.
22 Wewe utaufurahia uharibifu na njaa, na hutatishika na wanyama wakali wa nchi.
23 Kwa kuwa wewe utakuwa na mapatano na mawe ya shambani mwako, na wanyama wa mwituni watakuwa na amani na wewe.
24 Wewe utajua kwamba hema lako lina usalama; utatembelea zizi la kondoo wako na hutakosa kitu chochote.
25 Pia utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, na vizazi vyako vitakuwa kama nyasi ardhini.
26 Wewe utafika kaburini kwako mwenye umri kamili, kama vile rundo la mashuke ya nafaka liendavyo juu wakati wake.
27 Tazama, tumelipeleleza jambo hili; ndivyo lilivyo; lisikie, na ulifahamu kwa ajili yako mwenyewe.”