40
Yahweh aliendelea kuongea na Ayubu na kusema, “Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi? Na yeye anayehojiana na Mungu, na ajibu yeye.” Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, “ Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu. Ninazungumza mara moja, na sitakujibu; hakika, mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.” Kisha Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kusema, “Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume, kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu. Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki? Je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki? Je una mkono kama wa Mungu? Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye? 10 Jivike sasa katika utukufu na katika utu; jivalie mwenyewe heshima na enzi. 11 Sambaza ziada ya hasira yako; mtazame kila mmoja mwenye kiburi na umshushe chini. 12 Mwangalie kila mmoja mwenye kiburi na umweke chini; wakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama. 13 Wazike ardhini pamoja; zifunge nyuso zao katika sehemu zilizositirika. 14 Ndipo pia nitakapokubali ya kwamba mkono wako wa kulia waweza kukuokoa. 15 Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe. 16 Ona sasa, nguvu zake ziko katika viuno vyake; nguvu zake zi katika mishipa ya tumbo lake. 17 Yeye huuondoa mkia wake kama mti wa mwerezi; mishipa ya paja lake imeunganishwa pamoja. 18 Mifupa yake ni kama ya mirija ya shaba; na miguu yake ni kama kipande cha chuma. 19 Yeye ni mkuu wa viumbe vya Mungu. Ni Mungu pekee, ambaye alimwumba, anaweza kumshinda. 20 Kwa kuwa milima humpatia chakula; hayawani wa mashambani hucheza karibu. 21 Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope. 22 Miti yenye vivuli humfunika katika vivuli vyake; mierebi ya kijito inamzunguka pande zote. 23 Tazama, kama mto utazigharikisha kingo zake, hatikisiki; yeye anajiamini, hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake. 24 Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano, au kuichoma pua yake kwa mtego?