35
1 Aidha, Elihu aliendelea kusema,
2 “Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
3 Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
4 Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
5 Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
6 Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
7 Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
8 Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
9 Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
10 Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
11 ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
12 Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
13 Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
14 Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
15 Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
16 Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa.”