13
1 Tazama, jicho langu limeyaona haya yote; sikio langu limeyasikia na kuyaelewa hayo.
2 Kile mnachokifahamu, ndicho hicho mimi pia ninachokifahamu; Mimi siyo duni kwenu ninyi.
3 Hata hivyo, Mimi ningeweza kuzungumza na mwenye nguvu; Mimi natamani kusemezana na Mungu.
4 Lakini ninyi mnauficha ukweli kwa uongo; ninyi nyote ni tabibu msiokuwa na thamani.
5 Laiti, kwamba kwa pamoja mngeshikilia amani yenu! Hilo lingekuwa hekima yenu ninyi.
6 Sikia sasa kuhoji kwangu; Sikiliza kusihi kwa midomo yangu mwenyewe.
7 Ninyi mtazungumza visivyo haki kwa ajili ya Mungu, na ninyi mtazungumza udanganyifu kwa yeye? Ni kweli ninyi mngeonyesha ukarimu kwa yeye?
8 Ni kweli ninyi mngetetea katika mahakama kama mawakili wa Mungu?
9 Je, kweli ingekuwa vizuri kwenu wakati yeye akiwatafuta ninyi? Mngeweza ninyi kumdanganya yeye kama mlivyoweza kuwadanganya watu?
10 Yeye kwa hakika angewathibitisha upya ninyi ikiwa katika siri ninyi mmeonyesha kutokukamilika.
11 Je, ukuu wake usingewafanya ninyi muogope? Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?
12 Hadithi zenu za misemo ya kukariri, ni mithali zimetengenezwa kwa majivu; utetezi wenu ni utetezi uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.
13 Shikilieni amani yenu, mniache peke yangu, ili ya kwamba nipate kusema, acheni yaje yale yanayoweza kuja kwangu.
14 Nitaichukua nyama yangu mwenywewe katika meno yangu; Nitayachukua maisha yangu katika mikono yangu.
15 Tazama, ikiwa ataniua mimi, sitakuwa na tumaini lililobakia; hata hivyo, nitazitetea njia zangu mbele zake yeye.
16 Hiki kitakuwa sababu ya kutohesabiwa hatia, kwamba mimi sikuja mbele zake kama mtu asiyemcha Mungu.
17 Mungu, sikiliza kwa makini kuzungumza kwangu; ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.
18 Tazama sasa, Nimeuweka utetezi wangu katika mpangilio, Mimi ninafahamu kwamba mimi sina hatia.
19 Ni nani anayeweza kushindana na mimi katika mahakama? Ikiwa mlikuja kufanya hivyo, na kama mimi nilithibitishwa kukosea, ndipo ningekuwa kimya na kuyatoa maisha yangu.
20 Mungu, fanya mambo mawili kwa ajili yangu, na tena Mimi sitajificha kutoka katika uso wako.
21 Ondoa kutoka kwangu mkono wako unaotesa, na usiache utisho wako unifanye mimi kuogopa.
22 Ndipo niite mimi, na mimi nitakujibu; au uniache mimi niseme na wewe na wewe unijibu mimi.
23 Je, maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
24 Kwa nini unaficha uso wako kutoka kwangu mimi na kunitendea mimi kama adui yako?
25 Je, wewe utalitesa jani linalopeperushwa? Je, utaendelea kulifuatilia bua kavu?
26 Kwa maana wew unaandika chini vitu vichungu dhidi yangu mimi; wewe unanifanya mimi kurithi uovu wa ujana wangu.
27 Wewe pia unaiweka miguu yangu katika nguo nyembamba; wewe waangalia njia zangu zote; wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.
28 japokuwa mimi ni kama kitu kilichooza ambacho hutupwa mbali, kama vazi lile ambalo nondo wamelila.