3
Bwana akaniambia, “Nenda tena, mpendeni mwanamke, aliyependwa na mumewe; lakini ni mzinzi. Mpende kama mimi, Bwana, ninavyowapenda watu wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine na kupenda mikate ya zabibu.” Kwa hiyo nimemnunulia mwenyewe kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri. Nilimwambia, “Lazima uishi pamoja nami siku nyingi. Huwezi kuwa kahaba au kuwa na mtu mwingine yeyote. Kwa njia hiyo hiyo, nitakuwa pamoja nanyi.” Kwa maana wana wa Israeli wataishi kwa siku nyingi bila mfalme, mtu mkuu, dhabihu, nguzo ya mawe, efodi au sanamu za nyumbani. Baadaye watu wa Israeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Na katika siku za mwisho, watakuja wakitetemeka mbele za Bwana na wema wake.