9
1 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Nenda kwa Farao na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: “Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.”
2 Lakini ukikataa kuwaruhusu waende, kama utaendelea kuwa bakiza nyuma,
3 basi mkono wa Yahweh utakuwa kinyume dhidi ya mifugo yako shambani na kwa farasi, punda, ngamia, ng'ombe na kondoo, naitasababisha ugonjwa mbaya sana.
4 Yahweh ata tendea tofauti mifugo ya Israeli na mifugo Misri: Haukuna mnyama wa Waisraeli ataye kufa.
5 Yahweh ametenga muda; amesema, “Ni kesho ambapo nitafanya ilitukio katika nchi."”'
6 Yahweh akafanya hivi siku iliyofuata: mifugo yote ya Misri ikafa. Lakini hamna mnyama wa Waisraeli aliye kufa, hamna mnyama ata mmoja.
7 Farao akafanya utafiti, na tazama, hakuna mnyama ata mmoja aliye kufa. Lakini moyo wake ulikuwa mjeuri, hivyo hakuwaacha watu waende.
8 Kisha Yahweh akawambia Musa na Aruni, “Chukuwa majivu na uyajaze mkononi kutoka kwenye tanuru. Wewe, Musa, lazima uyarushe juu wakati Farao akitazama.
9 Yatakuwa vumbi safi nchi nzima ya Misri. Yatasababisha majipu na mafua kulipuka kwa watu na wanyama katika nchi yote ya Msri.”
10 Hivyo Musa na Aruni wakachukuwa majivu kutoka kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. KIsha Musa akarusha majivu juu. Majivu yakasababisha majipu na mafua kutokea kwa watu na wanyama.
11 Waganga hawakuweza kumzuia Musa kwasababu ya majipu, kwasababu majipu yalikuwa kwao na kwa Wamisri wote.
12 Yahweh akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, Farao hakuwasikiliza Musa na Aruni. Hili ndilo Yahweh alilo mwambia Musa Farao atalo fanya.
13 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Amka asubui mapema, simama mbele ya Farao, na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.
14 Kwa muda huu nitatuma mapigo kwako wewe, kwa watumishi wako na watu wako. Nitafanya hivi ili ujue hakuna kama mimi kwenye dunia yote.
15 Mpaka sasa ningeweza kuunyosha mkono wangu na kukushambulia wewe na watu wako kwa ugonjwa, na ungeondelewa kwenye nchi.
16 Lakini ni kwa sababu hii nimekuruhusu uishi: ili kukuonyesha nguvu zangu, ili kwamba jina langu litangazwe dunia nzima.
17 Bado unajiinua dhidi ya watu wangu kwa kuwaacha wasiende.
18 Sikiliza! Kesho muda kama huu nita leta mvua ya mawe ya barafu kubwa, kama ambayo haijawai kuonekana Misri toka ilipo anza hadi sasa.
19 Kisha sasa, tuma wanaume na ukusanye mifugo yako na vitu vyote ulivyo navyo mashambani sehemu salama. Kila mtu na mnyama aliyeko shambani na hajaletwa nyumbani - mawe ya barufu yatawashukia, na watakufa."”'
20 Kisha hao wa watumishi wa Farao walio amini ujumbe wa Yahweh waka harakisha kuleta watumwa na mifugo yao ndani ya nyumba zao.
21 Lakini hao ambao hawa kuchukuwa ujumbe wa Yahweh maanani waliacha watumwa wao na mifugo shambani.
22 Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu ili kuwe na mawe ya barafu katika nchi yote ya Misri, kwa watu, kwa wanyama, na kwenye mimea yote shambani na nchi nzima ya Misri.”
23 Musa akanyoosha mkono na gongo lake kuelekea mbiguni, na Yahweh akatuma mngurumo, mawe ya barafu, na radi kwenye nchi. Pia alinyesha mvua kwenye nchi ya Misri.
24 Hivyo kulikuwa na radi iliyo changanyika na mawe ya barafu, ilikuwa hatari sana, kuliko yeyote iliyowai kutokea kwenye nchi ya Misri tangu liwe taifa.
25 Katika nchi yote ya Misri, barafu ya mawe ilipiga kila kitu kwenye shamba, watu na wanyama. Ilipiga kila mmea shambani na kuvunja kila mti.
26 Isipo kuwa tu nchi ya Gosheni, walipo ishi Waisraeli, hapakuwa na mawe ya barafu.
27 Kisha Farao akatuma wanaume wakawaite Musa na Aruni. Akawaambia, “Nimetenda dhambi wakati huu. Yahweh ni mwenye haki, na mimi na watu wangu ni waovu.
28 Muombe Yahweh, kwasababu radi na barafu ya mawe imezidi. Nitawaacha muende, na hamtabaki tena hapa.”
29 Musa akamwambia, “Nitakapo ondoka tu kwenye mji, nitaitanua mikono yangu kwa Yahweh. Mngurumo utaacha, na hakutakuwa na barafu ya mawe tena. Kwa ili utajua kuwa nchi ni ya Yahweh.
30 Lakini kwa wewe na watu wako, najua bado hamu mheshimu Yahweh Mungu.”
31 Sasa kitani na shayiri ziliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa katika kukomaa, na kitani ilikuwa imestawi.
32 Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa mana zinachelewa kukua.
33 Musa alipo muacha Farao na mji, alitanua mikono yake kwa Yahweh; mngurumo na barafu ya mawe ikasimama, na mvua haikunyesha tena.
34 Farao alipoona mvua, barafu ya mawe, na mngurumo umekatika, akatenda dhambi na kufanya moyo wake kuwa mgumu, pamoja na watumishi wake.
35 Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, hakuacha watu wa Israeli waende. Hivi ndivyo Yahweh alimwambia Musa Farao atafanya.