40
1 Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
2 “Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka lazima wewe uandae hema la kukutania.
3 Utaweka sanduku la ushuhuda ndani yake, na utaziba sanduku kwa pazia.
4 Utaleta ndani meza na kuandaa kwa mpangilio vitu vyake. Kisha utaleta kinara cha taa na kuandaa taa.
5 Nawe utaweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na utaweka pazia katika mwingilio wa hema la kukutania.
6 Utaweka madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa mbele ya mwingilio wa hema ya kukutania.
7 Utaweka ile saani kubwa katikati ya hema la kukutania na madhabahu na utaweka maji ndani yake.
8 Uandae nyuani inayoizunguka, na utundike pazia katika mwingilio wa nyuani.
9 Lazima uchukuwe mafuta ya upako na upake hema la kukutania na kila kitu kilichopo ndani yake. Lazima uitenge na samani zake kwangu; kisha itakuwa takatifu.
10 Lazima upake mafuta madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake. Lazima utenge madhabhu kwa ajili yangu na itakuwa takatifu kwangu.
11 Upake mafuta beseni la shaba na sakafu yake na uitenge kwa ajili yangu.
12 Umlete Aruni na wanae kwa mwingilio wa hema la kukutania na uwaoshe wote kwa maji.
13 Utamfunika Aruni kwa mavazi yaliyo tengwa kwa ajili yangu, mpake mafuta na umtenge ili anitumikie kama kuhani.
14 Utawaleta wana wake na kuwafunika kwa nguo nzito.
15 Utawapaka mafuta kama ulivyo mpaka baba yao ili wanitumikie kama makuhani. Upako wao utawafanya makuhani wa kudumu vizazi vyote vya watu wao.”
16 Hivi ndivyo Musa alivyo sema; alifuata yote Yahweh aliyo muamuru. Alifanya vitu vyote hivi.
17 Hivyo hema la kukutania liliandaliwa siku ya kwanza ya mwezi wa mwaka wa pili.
18 Musa alianda hema la kukutania, akaeka sakafu zake sehemu yake, akaanda fremu zake, akashikisha chuma zake, na akaanda minara na nguzo zake.
19 Alitandaza mfuniko juu ya hema la kukutania na kuweka hema juu yake, kama Yahweh alivyo muamuru.
20 Alichukuwa amri za agano na kuweka kwenye sanduku. Pia aliweka nguzo kwenye sanduku na kuweka mfuniko wa kiti cha rehema.
21 Aliichukuwa sanduku na kuweka ndani ya hema la kukutania. Aliandaa pazia ili lizibe sanduku la ushuhuda, kama Yahweh alivyo muamuru.
22 Alieka meza kwenye hema la kukutania, kwa upande wa kaskazini mwa hema la kukutania, nje ya pazia.
23 Alieka mkate kwa mpangilio katika meza ya Yahweh, kama Yahweh alivyo amuru.
24 Alieka kinara cha taa kwenye hema la kukutania, upande wa pili wa meza, kusini mwa hema la kukutani.
25 Aliwasha taa mbele za Yahweh, kama Yahweh alivyo muamuru.
26 Aliweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba ndani ya hema la kukutania mbele ya pazia.
27 Alichoma uvumba wa manukato hapo, kama Yahweh alivyo muamuru.
28 Alitundika pazia katika hema ya kukutania.
29 Aliweka madhabahu ya sadaka ya kuteketeza katika hema ya kukutania. Aliitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka ya unga, kama Yahweh alivyo muamuru.
30 Aliweka beseni katikati ya hema ya kukutunia na madhabahu, na maji ya kuoshea.
31 Musa, Aruni, na wanae waliosha mikono yao na miguu kwenye beseni
32 muda wowote walipoenda kwenye hema ya kukutania na muda wowote walipoenda kwenye madhabahu. Walijisafisha, kama Yahweh alivyo muamuru Musa.
33 Musa alianda nyuani nyuma ya hema ya kukutania na madhabahu. Alianda pazia katika mwingilio wa nyuani. Katika hili, Musa alimaliza kazi.
34 Kisha wingu likafunika hema ya kukutania, na utukufu wa Yahweh ukafunika hema ya kukutania.
35 Musa hakuweza kuingia hema ya kukutania kwasababu wingu lilikuwa juu yake, na kwasababu utukufu wa Yahweh ulijaza hema ya kukutania.
36 Muda wowote wingu lilipo chukuliwa juu kutoka hema ya kukutania, watu wa Israeli waliendelea na safari yao.
37 Lakini kama wingu haliku nyanyuka juu kutoka hema ya kukutania, kisha basi watu hawaku safiri. Walibaki hadi siku lilipo nyanyuliwa juu.
38 Kwa kuwa wingu la Yahweh lilikuwa juu ya hema ya kukutania mchana, na moto wake ulikuwa juu yake usiku, wazi kwa watu wote wa Israeli kipindi chote cha safari yao.