35
1 Musa akawakusanya jamii yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndio mambo Yahweh aliyo waamuru mfanye.
2 Kwa siku sita kazi ya weza fanywa, lakini kwako, siku ya saba lazima iwe siku takatifu, siku ya Sabato ya mapumziko, takatifu kwa Yahweh. Yeyote atakaye fanya kazi hiyo siku lazima auawe.
3 Haupaswi kuwasha moto kwenye nyumba zenu siku ya Sabato.”
4 Musa akasema na jamii yote ya Waisraeli, kwa kusema, “Hichi ndicho kitu Yahweh alicho amuru.
5 Chukuwa sadaka kwa ajili ya Yahweh, wote wenye moyo mkunjufu. Leta sadaka kwa Yahweh - dhahabu, fedha, shaba,
6 buluu, zambarau, sufu nyekundu na kitambaa kizuri; nywele za mbuzi;
7 ngozi za kondoo zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo; na mbao za mshita;
8 mafuta ya taa kwa pahali patakatifu, viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa,
9 kwa uvumba mzuri na vito vya shohamu na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.
10 Kila mwanaume mwenye ustadi kati yenu aje na afanye kila kitu ambacho Yahweh aliyaamuru —
11 hema la kuabudia, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, nguzo, na sakafu;
12 pia sanduku na nguzo zake, kiti cha rehema, na pazia la kusitiri.
13 Walileta meza na miguu yake, vyombo vyake vyote, na mkate wa wonyesho;
14 kinara cha taa, vyombo vyake, taa, na mafuta ya zile taa;
15 ile madhabahu ya uvumba na nguzo zake, mafuta ya upako na uvumba ulitiwa maukato; kishikizo cha mwingilio wa hema ya kuabudia;
16 madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kitunzi cha shaba na nguzo na vyombo; na ile beseni kubwa na sakafu yake.
17 Walileta vishikizo kwa ajili ya nyuani na nguzo zake na sakafu yake, na pazia kwa ajili mwingilio wa nyauni;
18 na ile misumari ya hema la kuabudia na nyuani, pamoja na kamba zake.
19 Walileta mavazi yaliyofumwa kutumikia sehemu takatifu, mavazi takatifu ya Aruni kuhani na wanae, kwa wao kutumika kama makuhani.”
20 Kisha makabila yote ya Israeli yakaondoka na kwenda kutoka uweponi mwa Musa.
21 Kila mtu moyo wake ulimchochea na aliye andaliwa na roho yake alikuja na kuleta sadaka kwa Yahweh kwa matengenezo ya hema ya kuabudia, kwa vitu vyote kwajili ya huduma ndani yake, na kwa vazi takatifu.
22 Walikuja, wote wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa utayari. Walileta madini, hereni, pete, na vitu vya thamani, vitu vyote tofauti vyenye madini ya dhahabu. Waliwasilisha sadaka za dhahabu kama sadaka ya kupunga kwa Yahweh.
23 Kila mmoja alikuwa na sufu ya buluu, dhambarau, au nyekundu, nguo nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo zilizobadili kuwa nyekundu, na ngozi ya pomboo walivileta.
24 kila mmoja alitengeneza sadaka ya fedha au shaba walizileta kama sadaka kwa Yahweh, na kila mmoja aliyekuwa na mti wa mshita kwa matumizi ya kazi aliuleta.
25 kila mwanamke mwenye ustadi walisokota sufu kwa mikono yao na walileta sufu walizosokota za buluu, dhambarau, au sufu nyekundu, au nguo nzuri.
26 Wanawake wote wenye mioyo iliyochochewa na walio na ustadi walisokota singa za mbuzi.
27 Viongozi walileta mawe ya shohamu na mawe mengine kwaajili ya kuwekwa kwenye hiyo naivera na hicho kifuko cha kifuani;
28 walileta viungo na mafuta kwaajili ya taa, kwa mafuta ya upako, na kwa uvumba wa manukato.
29 Waisraeli walileta sadaka ya hiyari kwa Yahweh; kila mwanaume na mwanamke ambao mioyo yao ilikuwa tayari walileta vifaa kwaajili kazi zote ambazo Yahweh aliamuru kupitia Musa zifanyike.
30 Musa alisema kwa waisraeli, “Tazama, Yahweh ameita kwa jina juu ya Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huri, kutoka kabila la Yuda.
31 Aliijaza Bezaleli kwa Roho yake, kumpa hekima, uwelewa, na maarifa, kwa aina zote za ujenzi,
32 kufanya sanaa ya ubunifu na kufanya kazi za dhahabu, shaba, na shaba;
33 pia kukata na kupanga mawe na mbao iliochongwa- kufanya kazi za aina zote kwa ubunifu na ujenzi.
34 Aliiweka kufundisha ndani ya moyo wake, yeye pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, kutoka kabila la Dani.
35 Aliwajaza kwa ustadi wa kufanya kazi za aina zote, kufanya kazi ya kama kuchora mawe, kama mwerevu, kama mtia taraza katika nyuzi za rangu ya buluu, dhambarau, na nyekundu na nguo nzuri, na kama washonaji. Walikuwa wachonga mawe wa kazi zote, na walikuwa wabunifu wa sanaa.