29
Sasa Hivi ndivyo wapaswa kufanya kuwatenga ili wanitumikie kama makuhani. Chukuwa mtoto wa ng'ombe dume na kondoo bila lawama, mkate bila hamira, na keki bila hamira iliyo changanywa na mafuta. Pia chukuwa maandazi bila hamira yalio pakwa mafuta. Fanya maandazi kwa unga mzuri wa ngano. Lazima uweke kwenye ndoo moja, leta kwenye ndoo, na kuleta pamoja na ng'ombe dume na wana kondoo wawili. Lazima nawe umlete Aruni na wana wake wawili katika lango la kuingilia hema la kukutania. Lazima uwasafishe Aruni na wana wake kwenye maji. Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho ya naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi. Nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba. Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta. Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu. Nawe uwakaze mishipi, Aruni na wanawe, na kuwavika kofia. Nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu. 10 Kisha utamleta huyo ng’ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng’ombe. 11 Kisha utamchinja huyo ng’ombe mbele ya Yahweh pa hema ya kukutania. BWANA, 12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ng’ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu. 13 Kisha chukuwa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu. 14 Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi. 15 Pia mtwae kondoo mume mmoja; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo mume. 16 Kisha utamchinja huyo kondoo mume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kando-kando. 17 Kisha utamkata-kata kondoo vipande vyake, na kuyaosha matumbo yake na miguu yake, na kuiweka pamoja na vipande vyake na kichwa chake, 18 nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yaYahweh; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Yahweh kwa njia ya moto. 19 Kisha mtwae huyo kondoo mwingine; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo. 20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Aruni la upande wa kuume, na katika ncha za masikio ya kuume ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kuume, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kando-kando. 21 Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Aruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye. 22 Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu. 23 Utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya Yahweh. 24 Nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Aruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa-tikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh. 25 Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele yangu; ni sadaka iliyotengenezwa kwangu kwa njia ya moto. 26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahwe nacho kitakuwa ni sehemu yako. 27 Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Aruni na wanawe. 28 Navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Yahweh. 29 Na hayo mavazi matakatifu ya Aruni yatakuwa ya wanawe baada yake, wayavae watakapotiwa mafuta, na watakapowekwa kwa kazi takatifu. 30 Huyo mwanawe atakayekuwa kuhani badala yake atayavaa muda wa siku saba, hapo atakapoingia ndani ya hiyo hema ya kukutania, ili atumike ndani ya mahali patakatifu. 31 Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuitokosa nyama yake katika mahali patakatifu. 32 Na Aruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 33 Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu. 34 Na kwamba kitu cho chote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au cho chote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu 35 Ni hivyo utakavyowatendea Aruni na wanawe kama nilivyo kuagiza. Utawaweka kwa kazi takatifu siku saba. 36 Kila siku utamtoa ng’ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa. 37 Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu. 38 Lazima utoe kwenye madhabahu wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku 39 daima. Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni 40 Pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yenye kupondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji. 41 Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni. Nawe utamfanyia vivyo kama ile sadaka ya unga ya asubuhi, na kama ile sadaka yake ya kinywaji. Hii itatoa harufu nzuri, ni dhabihu ya kusongezwa kwangu kwa njia ya moto. 42 Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Yahweh, hapo nitakapokutana nanyi, ili niseme na wewe hapo. 43 Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo; na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu. Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu. 44 Pia Aruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 45 Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao. 46 Nao watanijua kuwa mimi ndimi Yahweh, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao. Ni mimi Yahweh, Mungu wao.