2
1 Hawa ndio watu katika jimbo waliochukuliwa mateka na kwenda na mfalme Nebukadneza, yeye aliwachukua utumwani Babeli, watu wakarudi katika miji yao ya Yerusalem na Yuda.
2 Walikuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari., Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndio idadi ya wanaume ya watu wa Israeli.
3 Waporoshi: 2, 172
4 Wana wa Shefatia: 372
5 Wana wa Ara: 775.
6 Wana wa Path-Moabu, kupitia Yeshua na Yoabu: 2, 812.
7 Wana wa Eliamu: 1, 254.
8 Wana wa Zatu: 945.
9 Wana wa Zakai: 760.
10 Wana wa Binui: 642.
11 Wana wa Bebai: 623.
12 Wana wa Azgadi: 1, 222.
13 Wana wa Adonikamu: 666.
14 Wana wa Bigwai: 2, 056.
15 Wana wa Adini: 454.
16 Wana wa Ateri kupitia Hezekiah: tisini na nane.
17 Wana wa Besai: 323.
18 Wana wa Harifu: 112.
19 Wanaume wa Hashimu: 223.
20 Wanaume wa Gibeoni: Tisini na tano.
21 Wanaume wa Bethlehemu: 123.
22 Wanaume wa Netofa: Hamsini na sita.
23 Wanaume wa Anathothi: 128.
24 Wanaume wa Beth-Azmawethi: Arobaini na mbili.
25 Wanaume wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi: Mia saba arobaini na tatu.
26 Wanaume wa Rama na Geba: 621.
27 Wanaume wa Mikmashi: 122.
28 Wanaume wa Betheli, na Ai: 223.
29 Wanaume wa Nebo: Hamsini na mbili.
30 Wanaume wa Magbishi: 156.
31 Wanaume wengine wa Elamu: 1, 254.
32 nne. Wanaume wa Harimu: 320.
33 Wanaume wa Lodi, na Hadidi, na Ono: 725.
34 Wanaume wa Yeriko: 345.
35 Wanaume wa Senaa: 3, 630.
36 Wana wa Yedaya kuhani wa nyumba ya Yoshua: 973.
37 Wana wa Imeri: 1, 052.
38 Wana wa Pashuri: 1, 247.
39 Wana wa Harimu: 1, 017.
40 Walawi: Wana wa Yeshua, na Kadmieli, wana wa Hodavia: Sabini na
41 nne. Waimbaji hekaluni wana wa Asafu: 128.
42 Walinzi: wana wa Shalumu, Ateri na, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai: 139 jumla.
43 Wale walichaguliwa kuhudumu ndani ya Hekalu: wana wa Siha, Hasufa, Tabaothi:
44 Keros, Siaha, Padoni.
45 Lebana, Hagaba, Akubu,
46 Hagabu, Salmai, Hanani
47 Wana wa Gideli, Gahari, Reaya,
48 Resini, Nekoda, Gazamu,
49 Uza, Pasea, Besai,
50 Asna, Meunimu, Nefusimu:
51 Wana wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri:
52 Basluthi, Mehida, Barsha:
53 Barkosi, Sisera, Tema:
54 Nesia, Tefa
55 Wana wa watumishi wa Selemani: Wana wa Sotai, Soferethi, Peruda,
56 Yaala, Darkoni, Gideli,
57 Shefatia, Hatili, Pokereth-Sebaimu, Amoni,
58 Walikuwa jumla ya watumishi mia tatu tisini na mbili waliochaguliwa kutumika katika Hekalu pamoja na wana wa watumishi wa Selemani.
59 Wale ambao walitoka Tel-mela, Tel-harsha, Kerubu, Adani, na Imeri, Lakini hawakuweza kuthibitisha kizazi chao kilitoka Israeli-
60 pamoja na mia sita hamsini na mbili wana wa Delaya, Tobia na Nekoda.
61 Vilevile, kutoka kwa wana wa kuhani: Wana wa Habaya, Hakosi, Barzilai {ambaye alipata mke kutoka kwa binti ya Barzilai, Mgileadi na akaitwa kwa jina lao}
62 Walitafuta kumbukumbu ya kizazi chao, lakini haikupatikana, hivyo wakaondolewa kwenye ukuhani kama wasiosafi.
63 Hivyo kiongozi akawakataza wasile kitu chochote kitakatifu kilichotakaswa mpaka kuhani mwenye Urimu na Thumimu athibitishe.
64 Jumla ya kundi 42, 360,
65 ukiondoa watumishi na wasaidizi (wao walikuwa 7, 337) waimbaji Hekaluni wanaume na wanawake (mia mbili)
66 Farasi wao: 736, Nyumbu wao: 245.
67 Ngamia wao: 435. Punda wao: 6, 720.
68 Walipokwenda kwenye nyumba ya Yahwe Yerusalem, wakuu wa mababa walijitoa kwa hiari kujenga nyumba.
69 Walitoa kadiri ya uwezo wao katika kufadhili kazi: Dhahabu za darkoni sitini na moja elfu, mane za fedha elfi tano na mavazi mia moja ya makuhani.
70 Basi makuhani na walawi, watu, waimbaji hekaluni, na walinzi wa getini, na wale waliochaguliwa kutumika katika Hekalu walikaa katika miji yao. Watu wote katika Israel walikuwa katika miji yao.