3
Kwa sababu ya hii mimi, Paulo, ni mfungwa wa Yesu Kristo kwa ajili yenu Mataifa. Na amini ya kwamba mmesikia juu ya kazi ya neema ya Mungu aliyo nipa kwa ajili yenu. Nawaandikieni kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu. Huu ni ukweli uliyofichika ambao niliandika kwa kifupi kwenye barua nyingine. Usomapo kuhusu haya, utaweza kutambua busara yangu katika ukweli huu uliofichika kuhusu Kristo. Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa wana wa watu. Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho kwa Mitume waliotengwa na Manabii. Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili. Na kwa hili nimefanyika mtumishi kwa zawadi ya neema ya Mungu iliyotolewa kwangu kupitia utendaji wa nguvu yake. Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote katika wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo. inanipasa kuwaangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote. 10 Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu. 11 Haya yangetokea kupitia mpango wa milele ambao aliukamilisha ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu. 12 Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake. 13 Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwasababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu. 14 Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba. 15 ambaye kwa yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina. 16 Ninaomba kwamba apate kuwanemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu. 17 Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani. 18 Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo. 19 Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu. 20 Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu, 21 kwake yeye kuwe utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina.