18
Makuhani, ambao ni Walawi, na makabila yote ya Lawi, hayatakuwa na mgao wala urithi pamoja na Israel; wanapaswa kula dhabihu ya Yahwe iliyotengenezwa kwa moto kama urithi wao. Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Yahwe ni urithi wao, kama alivyosema nao. Hii ni sababu ya makuhani kutoka kwa watu, kutoka kwa wale wanaotoa dhabihu, kama itakuwa ng'ombe au kondoo: wanapaswa kutoa kwa kuhani bega, mashavu mawili, na sehemu za ndani. Mazao ya kwanza ya nafaka zako, mvinyo wako mpya, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, unapaswa umpe. Kwa kuwa Yahwe Mungu wako amemchagua kutoka kwenye makabila yote yako kusimama kutumika kwa jina la Yahwe, yeye na wana wake milele. Kama Mlawi anatoka kati ya miji yenu nje ya Israel yote kutoka ambapo anaishi, na utamani kwa moyo wake wote kuja katika eneo Yahwe atachagua, basi anapaswa kutumika kwa jina la Yahwe Mungu wake kama ndugu zake wote Walawi wanafanya, wanaosimama mbele ya Yahwe. Wanapaswa kuwa na mgao wa kufanana wa kula, badala ya kile kinachokuja kutokana na mauzo ya urithi wa familia yake. Wakati mmekuja katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, mnapaswa kujifunza kuangalia machukizo ya mataifa. 10 Pasipatikana miongoni mwenu mmoja anayemweka kijana wake au binti yake kwenye moto, yeyote anatumia uganga, yeyote anatabiri, au mchawi, mchawi yeyote, 11 yeyote aongeae na wafu, au yeyote aongeae na roho. 12 Kwa yeyote afanyae mambo haya ni chukizo kwa Yahwe; ni kwa sababu ya machukizo haya ambayo Yahwe Mungu wenu anawaondosha mbele zenu. 13 Mnapaswa kuwa wakamilifu mbele ya Yahwe Mungu wenu. 14 Kwa mataifa haya ambayo mtayafukuza kusikiliza wale wafanyao uchawi na uganga; lakini kwenu, Yahwe Mungu wenu amewakataza ninyi kufanya hivyo. 15 Yahwe Mungu wenu atainua kwa ajili yenu nabii kutoka miongoni mwenu, mmoja wa ndugu zenu, kama mimi. Mnapaswa kumsikiliza. 16 Hiki ndicho mlichouliza kutoka kwa Yahwe Mungu wenu huko Horebu katika siku ya kusanyiko, kusema, “Acha tusisikie tena sauti ya Yahwe Mungu wetu, wala kuona moto mkuu tena, wala tutakufa.” 17 Yahwe alisema nami, “Kile walichosema ni kizuri. 18 Nitamwinua nabii kwa ajili yao kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe. Nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, na ataongea nao yote niliyowakuamuru. 19 Itakuwa kama yeyote hatasikia maneno yangu ambayo anazungumza kwa jina langu, nitalitaka kwake. 20 Lakini nabii ambaye anazungumza neno kwa kiburi kwa jina langu, neno ambalo sijamuamuru kusema, au ambaye anayezungumza kwa jina la miungu mingine, huyo nabii atakufa. 21 Hivyo ndivyo unapaswa kusema katika mioyo yenu: “Tutagunduaje kuwa ujumbe ambao Yahwe hajazungumza? 22 Mtagundua ujumbe ambao Yahwe amezungumza pindi nabii azungumzapo kwa jina la Yahwe. Kama hiyo haitokei wala kufanyika, basi hicho ni kile ambacho Yahwe hajazungumza na nabii amezungumza kwa kiburi, na hampaswi kumuogopa.