7
Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana: Danieli alieleza, “Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu. Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari. Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, lakini alikuwa na mabawa ya tai. Nilipokuwa natazama, mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu. Na alipewa akili za kibinadamu. Na kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu, na alikuwa ameinama, alikuwa na mbavu tatu katikati ya meno yake katika mdomo wake. Aliambiwa, 'Inuka na umeze watu wangi.' Baada ya hili, niliangalia tena. Kulikuwa na mnyama mwingine ambaye alionekana kama chui. Mgongoni mwake alikuwa na mabawa manne kama mabawa ya ndege, na alikuwa na vichwa vinne. Alipewa mamlaka ya kutawala. Baada haya, niliona usiku katika ndoto yangu mnyama wa nne, mwenye kuogofya, na kutisha na mwenye nguvu. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; aliteketeza, na kuvunja vunja katika vipande, na kusaga saga katika miguuni pake kile kilichosalia. Alikuwa ni wa tofauti na wanyama wengine, na alikuwa na pembe kumi. Na wakati nilipokuwa natafakari juu ya pembe, nilitazama na niliona pembe nyingine ndogo ilichipuka katikati ya pembe zingine. Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa. Niliona katika pembe hii macho kama macho ya mtu na mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa. Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto. 10 Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na mamilioni ya watu walimtumikia, na wengine mia moja milioni walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa. 11 Niliendelea kuangalia kwasababu ya maneno ya kiburi yaliyosemwa na pembe. Nilitazama wakati mnyama anauliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto. 12 Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda. 13 Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake. 14 Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa. 15 Na kwangu mimi, Danieli, roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua. 16 Nilimsogelea mmoja wa hawa walikuwa wamesimama hapo na nikamwomba anioneshe maana ya mambo haya. 17 Hawa wanyama nne wakubwa ni wafalme wanne ambao watatoa katika nchi. 18 Lakini watu watakatifu wa Mungu aliyejuu wataupokea ufalme na wataumiliki milele na milele.' 19 Ndipo nilipotaka kujua zaidi juu ya mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti sana na wengine na alikuwa wa kutisha pamoja na meno yake ya chuma na makucha ya shaba; alimeza, na alivunja vipande vipande, na alisaga saga kwa miguu yake kile kilichokuwa kimesalia. 20 Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliokuwa unajisifu kwa mambo makubwa na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine. 21 Na nilipotazama, pembe hii iliinua vita dhidi ya watu watakatifu na ilikuwa inawawashinda mpaka pale 22 Mzee wa Siku alipokuja, na watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana. Ndipo wakati ulipowadia ambapo watu watakatifu waliupokea ufalme. 23 Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande. 24 Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu. 25 Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana na atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka. 26 Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa. 27 Ufalme na utawala, ukubwa wa falme chini ya mbingu yote, watapewa watu walio wa watu watakatifu wa Yeye Aliye juu Sana. Ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zingine zote zitamtumikia na kumtii yeye.' 28 Na huu ndio mwisho wa mambo. Na kuhusu mimi, Danieli, mawazo yangu yanihuzunisha sana mimi na mwonekano wa uso wangu ulibadilika. Lakini mambo haya niliyahifadhi mimi mwenyewe.”