4
1 Lisikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani, ninyi mliomo katika mlima wa Samaria, ninyi mnaowakandamiza maskini, ninyi mnaowaponda wahitaji, ninyi muwaambiao waume zenu, “Tuleteeni vinywaji.”
2 Bwana Yahwe ameapa kwa utukufu wake, “Tazama, siku zitakuja kwenu wakati watakapowaondoa kwa ndoana, wa mwisho wenu na ndoana za kuvulia samaki.
3 Mtatoka kupitia mahali palipo bomolewa kwenye kuta za mji, kila mmoja wenu kwenda moja kwa moja kupitia hapo, na mtajitupa mbele ya Harmoni -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.”
4 “Nendeni Betheli na uovu, hata Gilgali mkaongeza dhambi, leteni dhabihu zenu kila asubuhi, zaka zenu kila baada ya siku tatu.
5 Toeni dhabihu za shukurani pamoja na mkate; tangazeni sadaka za hiari; watangazieni, kwa kuwa hii ndiyo iwapendezayo, ninyi watu wa Israeli -hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
6 Nawapatia usafi wa meno katika miji yenu na na kupungukiwa na mkate katika sehemu zenu zote. Bado hamkurudi kwangu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
7 Pia nimeizuia mvua kutoka kwenu wakati bado kulikuwa na miezi mitatu kwa mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji, na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
8 Walizunguka miji miwili au mitatu kwenda mji mwingine kunywa maji, lakini hawakutosheka. Bado hawakunirudia mimi -asema Yahwe.
9 Nimewapiga kwa maradhi yanayosababisha kuvu. Wingi wa bustani, mashamba yenu ya zabibu, mitini yenu, na mizaituni-kuteketeza yote. Bado hamkunirudia hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
10 Nimetuma tauni kwenu kama ya Misri. Nimewaua watoto wenu kwa upanga, kubeba farasi zenu, na kuufanya uvundo wa kambi zenu na kuingiza kwenye pua zenu. Bado hamkunirudia mimi -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
11 Nimeiangamiza miji miongoni mwenu, kama wakati Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijinga kilichonyakuliwa kutoka kwenye moto. Bado hamkunirudia - asema Yahwe.
12 Kwa hiyo nitafanya jambo baya kwako, Israeli; na kwa sababu nitafanya jambo baya kwako, jiandae kukutana na Mungu, Israeli!
13 Kwa kuwa, tazama, yeye atangenezaye milima pia ndiye aumbaye upepo, humfunulia mawazo yake mwanadamu, hufanya asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahala pa juu ya dunia. Yahwe, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.”